Chuo kikuu cha sokoine cha kilimo kwa kupitia idara ya sayansi ya wanyama,viumbe maji na malisho kimeandaa mafunzo ya ufugaji wa samaki yatakayofanyika kuanzia tarehe 02/05/2018 hadi tarehe 05/05/2018 katika ukumbi wa ICE uliopo kampasi kuu ya SUA.
Ili kushiriki katika mafunzo haya mshiriki anatakiwa
- Awe na uhitaji endelevu na nia ya dhati ya kutaka kufuga samaki
- Aliyeanza kufuga na anataka kupata mbinu za ufugaji zaidi
Idadi ya washiriki ni watu 30 tu, watakaowahi kuchukua fomu na wenye nia ya dhati ya kufuga samaki ndio watakaopewa kipaumbele.Mshiriki atajigharamia usafiri, malazi pamoja na chakula cha jioni
Fomu zinapatikana SUAMEDIA na ICE kampasi kuu ya SUA,
Mafunzo ni bure wote mnakaribishwa,
Kwa mawasiliano zaidi piga simu namba 0768503292 au 0754370047,
Kwa wanaotoka mbali, hostel zipo ICE SUA kwa bei nafuu kabisa.