SUA Mshiriki Kongamano la Kiswahili Nchini Uganda

Vijana kama nguvu kazi ya maendeleo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wametakiwa kujifunza, kuipenda na kuisambaza lugha ya Kiswahili ili kuifanya jumuiya hiyo kuwa imara na kudumisha umoja kwa nchi zote. Wito huo umetolewa na Mhadhiri Mwandamizi na Mkuu wa Idara ya Taaluma za Lugha kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo  Dkt. Onesmo Nyinondi wakiti akitoa wasilisho lake kwenye kongamano la kwanza la kimataifa la Kiswahili lililofanyika kwenye uwanja wa taifa wa sherehe za uhuru Kololo Kampala nchini Uganda.