TANGAZO LA MAFUNZO YA MUDA MFUPI YA UFUGAJI WA SAMAKI

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kupitia Taasisi ya Elimu ya Kujiendeleza (ICE) na Idara ya Sayansi za wanyama, ufugaji wa viumbe majini na nyanda zamalisho kimeandaa mafunzo ya ufugaji wa samaki yatakayofanyika mwezi wa tano, 2019.

ufugaji samaki


Tarehe ya mafunzo : 06/05/2019 hadi tarehe 09/05/2019 kuanzia saa mbili asubuhi hadi alasiri.

Mahali: Ukumbi wa Taasisi wa Elimu ya Elimu ya Kujiendeleza (ICE) uliopo kampasi kuu ya SUA.

Malengo ya mafunzo :Baada ya kumaliza mafunzo mshiriki ;

  • Ataelewa dhana ya ufugaji bora wa samaki
  • Atapata elimu na ujuzi wa ufugaji mseto wa samaki
  • Atapata elimu na ujuzi wa jinsi ya kujenga bwawa la samaki, na jinsi ya kurutubisha bwawa
  • Ataelewa jinsi ya kusafirisha na kupandikiza samaki kwenye bwawa
  • Atapata ujuzi wa kutengeneza chakula cha samaki na kuwalisha samaki
  • Atapata elimu na ujuzi wa kuvua samaki kwenye bwawa
  • Atapata elimu ya kutunza kumbukumbu na umuhimu wake

Aina ya Mafunzo: Mafunzo yatafanyika kwa nadharia na vitendo

Walengwa: Mtu yeyote mwenye nia ya kufuga samaki na aliyeanza kufuga ili kupata mbinu zaidi

Ada ya ushiriki:Hakuna ada ya mafunzo. Mshiriki atajigharamia gharama zote za kujikimu wakati wamafunzo ikiwemo usafiri, malazi, chakula, na kununua kitini cha mafunzo, n.k.

Idadi : Washiriki  30

Vyeti vya kuhitimu:  Mwisho wa mafunzo, mshiriki atatunukiwa cheti cha kushiriki mafunzo

Jinsi ya kuomba: Mwombaji atajaza fomu iliyoambatanishwa hapa chini au anaweza kufika katika ofisi ya Taasisi ya Elimu ya Kujiendeleza (ICE).

Kwa watakao hitaji huduma ya Hostel inapatikana ICE, SUA kwa bei nafuu.

Kwa mawasiliano zaidi :

Piga simu namba +255768503292; +255789345122

Barua pepe: babhili@yahoo.com(link sends email);  ibabili@sua.ac.tz(link sends email)

Nakala kwa: saudakanjanja@sua.ac.tz(link sends email)

Bofya hapa kupakua fomu ya maombi

 

Share this page