Elimika, Burudika na SUAMEDIA

Ugani (Outreach) ni moja ya majukumu makuu manne ya Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo (SUA), ambayo hujumuisha mafunzoutafiti na huduma kwa jamii. Chuo hiki hutekeleza majukumu yake ya ugani kupitia Taasisi ya Elimu ya Kujiendeleza (ICE), ambayo ndiyo kiungo kati ya SUA na wadau mbalimbali ndani na nje ya Chuo.

Taasisi ya ICE iliyoanzishwa mwaka 1988 kupitia Tangazo la Serikali Na.25 inaundwa na vitengo vitatu kama ifuatavyo;

  1. UganiElimu ya Kujiendeleza na Elimu kwa Jamii (Outreach, Continuing and Community Education); 
  2. Huduma za kumbi za mikutano (Conference Services); na
  3. Vyombo vya Habari za Elimu (Education Communication Media). 

SUAMEDIA hufanya kazi chini ya kitengo kilichotajwa hapo mwishoni. Kitengo hiki ni kati ya nyenzo muhimu ambazo ICE na SUA kwa ujumla hutumia katika kutekeleza majukumu ya ugani. 

Sokoine University of Agriculture TV and Radio

Historia ya SUAMEDIA inaanzia mwaka 1994 wakati Chuo kilipoanzisha televisheni iitwayo SUATV.  Miaka 11 baadaye (yaani mwaka 2015), Chuo kilianzisha redio ya masafa ya FM (SUAFM Radio), hivyo jina likabadilishwa kutoka SUATV kuwa SUAMEDIA.

Endelea...

Share this page