Washiriki wa kikao kazi cha utekelezaji wa Mradi wa Utafiti wa Majaribio kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) pamoja na VETA Dodoma, wamekutana kujadili mikakati ya kukuza ujuzi wa kidigitali kwa vijana ili kuwawezesha kujiajiri au kuajiriwa.
Prof. Maulid Mwatawala

Mradi huo unalenga kuwajengea vijana uwezo wa kutumia elimu kuhusu teknolojia za kidigitali kama nyenzo ya kujikwamua kiuchumi, sambamba na kuonesha fursa zinazotokana na maendeleo ya teknolojia ya kidigitali.
Akizungumzia Mradi, Kiongozi wa Mradi huo, π«ππ. π¨πππππ π π©ππππππππππ kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia amesema Mradi unaenda kuwawezesha vijana elimu ya fursa za teknolojia kwa kipindi cha miezi mitatu, kisha kutathmini ufanisi wa elimu itakayotolewa kulingana na vijana watakavyofanya kazi baada ya uwezeshaji huo.
Akifungua kikao kazi hicho, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo - Taaluma, Prof. Maulid Mwatawala, amesema taasisi zinazoshiriki katika mradi huo zinapaswa kuhakikisha kuwa vijana wanaoishi katika jamii zinazozunguka vyuo hivyo wanakuwa wa kwanza kunufaika na mafunzo hayo, ili wawe kielelezo kwa wengine.
Β
Ameongeza kuwa maendeleo ya kidigitali yameleta fursa nyingi za kiuchumi, ambapo vijana wanaweza kujiajiri kupitia ubunifu wa mawazo na miradi mbalimbali, hali itakayowawezesha kupata ufadhili kutoka kwa wadau tofauti.
Mradi wa utekelezaji wa utafiti wa majaribio katika teknolojia ya kidigitali kwa vijana unafadhiliwa na Benki ya Dunia ukilenga kuwaonesha vijana wa kitanzania fursa zinazopatikana kwa matumizi ya teknolojia mbalimbali za kidigitali.
Β
Β
Β