MBASHARA: https://www.youtube.com/live/gzD6yZSTtjs
Kwa niaba ya Menejimenti nampenda kuwataarifu kuwa siku ya Ijumaa tarehe 06 Desemba, 2024 kuanzia saa 8:00 mchana katika Ukumbi wa Multipurpose, Kampasi ya Edward Moringe, Morogoro tutakuwa na Kongamano la Miaka 63 ya Uhuru wa Tanganyika.
Mada Kuu katika Kongamano hilo ni:-
- Kilimo chetu, tulipotoka tulipo na mustakabali wa Tanzania bora
- Uwekezaji kwenye Kilimo kinachohimili mabadiliko ya tabianchi
- Kilimo biashara na mbinu za kisasa kuelekea mapinduzi ya nne ya viwanda
- Kilimo cha kisasa, ushiriki wa vijana na hatma ya mageuzi ya uchumi wa nchi
- Maono na uthabiti wa serikali ya awamu ya sita katika kuibua fursa mpya katika kilimo
Miongoni mwa watoa mada katika Kongamano hilo ni pamoja na Bw. Husein Omar Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Prof. Daniel Ndyetabula, Mhadhiri SUA, Dkt. Yasinta Nzogela, Mhadhiri SUA na Bw. Juma Haji, Afisa Mwandamizi, Uvuvi wa Bahari Kuu.
Karibuni tushiriki bila kukosa.