Dkt. Buriani Awapongeza SUA kwa Tafiti za Kilimo,Mifugo na Uvuvi

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Dkt. Batilda Buriani amekipongeza Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo SUA Kwa kufanya Tafiti zenye tija katika sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi na kuongeza uchumi wa Watanzania kupitia sekta hizo.

 

Dkt. Buriani Awapongeza SUA kwa Tafiti za Kilimo,Mifugo na Uvuvi

Ametoa pongezi hizo Agosti 2, 2024 wakati akifungua Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Mashariki katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mkoani Morogoro yaliyobeba kauli mbiu isemayo “Chagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi".

 

GUDbmZBXIAABIGo

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo- Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu Prof. Maulid Mwatawala 𝐚𝐤𝐢mweleza Mhe. Batilda Burian, RC Tanga shughuli 𝐳𝐢𝐧𝐚𝐳𝐨𝐨𝐧𝐞𝐬𝐡𝐰𝐚 na SUA kwenye ya Maonesho ya Sikukuu ya Nanenane 2024 𝐕𝐢𝐰𝐚𝐧𝐣𝐚 𝐯𝐲𝐚 𝐉𝐮𝐥𝐢𝐮𝐬 𝐍𝐲𝐞𝐫𝐞𝐫𝐞

Dkt. Buriani amesema SUA imetumia mabadiliko ya tabianchi kama fursa kwa kufanya tafiti mbalimbali zinazosaidia kuendeleza kilimo nchini

Aidha amewataka wakulima na wafugaji kutumia fursa ya maonesho hayo kwa kutembelea Maonesho ya nanenane kujifunza vitu vipya kama nyasi za malisho, teknolojia ya upimaji wa udongo, miundombinu ya umwagiliaji kwani nchi haijaweza kutumia fursa kikamilifu kutokana na mabadiliko ya tabianchi ambayo husababisha ukame, mafuriko na kuongezeka kwa joto.

WhatsApp Image 2024-08-02 at 23.11.19

Pia amewapongeza wakulima na wavuvi ambao wamejitoa kushiriki Maonesho ya Nane Nane mwaka huu na kusema kuwa ushiriki wao utasaidia kuongeza ujuzi, uwezo na mawazo tofauti kutokana na kukutana na wadau wengine kupitia maonesho hayo kama lengo lake la kutoa elimu na kuongeza wafugaji na wavuvi na wadau wengine katika mnyororo wa thamani.

Kwa upande wao wananchi waliopata fursa ya kutembelea mabanda na kijifunza teknolojia za Kilimo, mifugo na Uvuvi wamesema wamepata elimu itakayowasaidia katika shughuli zao za Kila siku.

Share this page