Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mgeni wake Rais wa Romania Mhe. Klaus Iohannis washuhudia utiaji Saini wa Mikataba ya Ushirikiano ikiwemo Mkataba uliotiwa saini na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Prof. Raphael Chibunda na Waziri wa nchi wa Masuala ya Dunia na Mikakati ya Kidiplomasia wa Romania Mhe. Traian Laurentiu Hristea.
Hafla hiyo ya Utiaji wa Saini Mkataba wa Ushirikiano baini ya Tanzania na nchi ya Romania imefanyika Novemba 17, 2023 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
"Uhusiano wa Romania na Tanzania ulianza May 1964 yaani mwezi mmoja tu baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Romania imekuwa mbia wetu kama Nchi na kama Nchi Mwanachama wa Umoja wa Ulaya hivyo ni dhamira yetu kuendelea kudumisha umoja huu" - Rais Samia Suluhu Hassan.
"Tumezungumzia wigo wa kuongeza ufadhili wa masomo hususani kwenye fani za Udaktari na Ufamasia, pia katika kudumisha uhusiano, Romania imekubali kwa mwaka huu kutoa nafasi 10 za masomo kwa Watanzania katika maeneo tutakayoyachagua" - Rais Samia Suluhu Hassan.