Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imewapongeza wahitimu bora wa Chuo Kikuu cha Kilimo Cha Sokoine (SUA) cha Morogoro kwa kuwapatia zawadi ya fedha taslimu shilingi milioni Tano (5). Motisha hiyo ya fedha, imetolewa na TADB kama sehemu ya kuwapongeza wanafunzi waliofanya vizuri zaidi kupitia mpango mkakati wake mpya uliozinduliwa mwaka huu.
Akiongea wakati wa hafla ya kutoa zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri na wafanyakazi katika eneo la utafiti, Afisa Rasilimali Watu Mkuu wa TADB Bi. Jacqueline Minja alisema hatua hiyo ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za serikali inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Kilimo Cha Sokoine (SUA) kampasi kuu Morogoro, Prof Raphael Chibunda (katikati) akiongea na Afisa Rasilimali Watu Mkuu wa Benki ya maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Bi. Jacqueline Minja (kushoto) pamoja na wafanyakazi wengine wa TADB na SUA ofisini kwake.
Afisa Rasilimali Watu Mkuu wa Benki ya maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Bi. Jacqueline Minja (kushoto) akimkabidhi zawadi Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Kilimo Cha Sokoine (SUA) kilichopo mkoani Morogoro Prof Raphael Chibunda muda mfupi baada ya kumtembelea ofisini kwake na kufanya mazungumzo ya namna taasisi hizo mbili zinaweza kuendelea kushirikiana kuboresha sekta ya kilimo hapa nchini
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo ( wa pili kushoto) , Afisa Rasilimali Watu Mkuu wa Benki ya maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Bi. Jacqueline Minja (wa tatu kushoto), wakikabidhi mfano wa hundi kwa wahitimu bora Kumi (10) wa Chuo Kikuu Cha Kilimo Cha Sokoine (SUA). Wanaoshuhudia kushoto ni Makamu Mkuu wa chuo SUA Prof Raphael Chibunda na kulia ni baadhi ya wafanyakazi wa TADB.
Wafanyakazi wa Benki ya maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) wakifurahi katika picha ya pamoja na baadhi ya wahitimu bora wa Chuo Kikuu Cha Kilimo Cha Sokoine (SUA) waliofanya vizuri zaidi katika masomo yao muda mfupi baada ya benki hiyo kukabidhi zawadi ya fedha taslimu shilingi milioni 5 kwa wanafunzi hao kuwapongeza kwa juhudi walizoonesha katika masomo yao.
Afisa Rasilimali Watu Mkuu wa Benki ya maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Bi. Jacqueline Minja (katikati) akiongea na baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Kilimo Cha Sokoine (SUA) waliofanya vizuri zaidi katika masomo yao muda mfupi baada ya benki hiyo kukabidhi zawadi ya fedha taslimu shilingi milioni 5 kwa wanafunzi hao ikiwa ni kama motisha.
https://www.michuzi.co.tz/2023/11/tadb-yawashika-mkono-wahitimu.html