SUA kukarabati Jengo lililomilikiwa na Wajerumani ili kutumika kwa shughuli za Utalii, Mafunzo kwa Wanafunzi wa Shahada ya Utalii

Katika kuhakikisha Sekta ya Utalii inakua na kuleta tija hapa nchini, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), kupitia Ndaki ya Misitu, Wanyamapori na Utalii pamoja na Kurugenzi ya Miliki na Kazi kimeweza kukagua ukarabati wa jengo lililopo eneo la Morning Sight katika Safu ya Milima ya Uluguru. Jengo hili hutumika kwa shughuli za utalii.

 

SUA kukarabati Jengo lililomilikiwa na Wajerumani ili kutumika kwa shughuli za Utalii, Mafunzo kwa Wanafunzi wa Shahada ya Utalii

 

DSC 0391 0

Dkt. Agnes Sirima ambaye ni Kaimu Rasi wa Ndaki ya Misitu, Wanyamapori na Utalii amesema jengo hilo lilikuwa likimilikiwa na Wajerumani lakini kwa sasa linamilikiwa na SUA chini ya usimamizi wa Idara ya Utalii na Mapumziko huishi, Ndaki ya Misitu, Wanyamapori na Utalii.

 Mbali na kuwa kivutio na eneo linalotumika kwa shughuli za utalii, Idara inatumia eneo hilo kama moja ya kituo cha mafunzo kwa wanafunzi wa shahada ya Utalii. 

“ Jengo lina ukubwa wa vyumba sita vinavyoweza kutumika kwa malazi kwa wageni wasiopenda kupiga kambi (camping).   Eneo hili pia linatoa muonekano mzuri wa mji wa Morogoro hasa nyakati za usiku”, amesema  Dkt. Sirima.

Ameongeza kuwa mara baada ya kumalizika na kuanza kutumika kwa jengo hilo fursa nyingi zitaongezeka kwa wanajamii wanaozunguka eneo hilo.  

Kwa upande wake Bw. Salim Singo kutoka Kurugenzi ya Miliki na Ujenzi ambaye ni Msimamizi Mkuu katika ukarabati wa ujenzi wa jengo hilo amesema tangu kujengwa kwa jengo hilo mwaka 1911 halijawahi kufanyiwa ukarabati lakini Chuo kwa kuona umuhimu wa jengo hilo kimeweza kufanya ukarabati huo ili kuweza kuendelea kuwavutia watalii kutoka sehemu mbalimbali ulimwenguni. 

Ameongeza kuwa ukarabati huo utakapokamilika itakuwa ni faida kwa Chuo kwa kuwa kitaweza kuongeza mapato kutokana na watalii watakaoweza kufika maeneo hayo.

DSC 0478

 

DSC 0494

DSC 0486

DSC 0473

DSC 0422

DSC 0379 (1)

DSC 0345

DSC 0510 (1)

Share this page