Documentary: Mafanikio ya mradi wa RIPAT SUA


Kilimo ni moja kati ya shughuli ambayo inaajiri watu wengi kuliko shughuli zingine barani afrika, na kwa Tanzania kinatoa ajira za zaidi ya asilimia 70 ya watanzania nah ii kutokana na watu wengi zaidi kukitegemea katika kupata chakula na kujikwamua kutoka katika wimbi la umasikini.

Asilimia kubwa ya Watanzania wanaotegemea kilimo ni wakulima wadogo wadogo lakini  kinaonekana kuwa ndio uti wa mgongo wa uchumi wa watanzania ingawa bado tija imeendelea kuonekana kuwa ndogo kutokana na sababu mbalimbali.

Jitihada kubwa zimekuwa zikifanywa na serikali pamoja na wadau wengine wa sekta hiyo katika kuongeza tija  lakini  hakijafikia kwenye kiwango kinachokubalika pamoja na kuwepo kwa tafiti nyingi zinazotoa matokeo ya kisayansi yanayojibu changamoto hizo nchini.

Kwa kutambua umuhimu wa Kilimo katika ustawi wa jamii na Taifa kwa ujumla mnamo mwezi june mwaka 2014 Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa kushirikiana na Shirika la RECODA lenye makao yake makuu jijini Arusha wakaanzisha mradi wa Uhakiki wa usambazaji wa teknolojia kupitia mfumo wa Jitihada shirikishi za kuleta mageuzi ya kilimo vijijini RIPAT SUA kwa ufadhili wa TOM KELAR na BLUE MASH Society kutoka Denmark.

Makala hii inalenga kuonesha utelezaji wa mradi huu kuanzia mwanzo hadi mwisho na mafanikio yake. 

RIPAT

Share this page