Wajumbe wa kamati ya ukaguzi wa ndani SUA wajengewa uwezo

Wajumbe wa Kamati ya Ukaguzi ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) wamekumbushwa kufuata sheria, taratibu na miongozo inayotolewa ya kamati hiyo  ili kuboresha ufanisi wa kazi na kutimiza malengo ya Chuo

SUA

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) (katikati waliokaa kwenye viti) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ya ukaguzi wa ndani na nje ya Chuo na Menejimenti ya Chuo wakati wa Mafunzo ya kamati ya ukaguzi SUA

Hayo yamesemwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Prof. Raphael Chibunda  wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa kamati ya Ukaguzi wa ndani ya Chuo iliyofanyika ukumbi wa Kituo cha kuratibu hewa ya ukaa Katika Kampasi ya Edward Moringe Morogoro.

“Mimi ninamatumaini makubwa kwamba sisi sote tunaoshiriki mafunzo haya tutakuwa  wasikivu na tutajipa muda ili kuelewa na kukubali kukumbushwa majukumu na umuhimu wa shughuli za ukaguzi katika kusimamia majukumu ya Chuo” amesema Prof. Chibunda.

Prof. Chibunda amesema kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya Utekelezaji wa Mpango kazi wa Kamati ya Ukaguzi ya mwaka wa fedha 2021/2022 na ni sehemu ya kutekeleza hati Idhini ya kamati kuwa yatolewe mafunzo mafupi kwa wanakamati wa kamati ya ukaguzi.

“Kama wengi wetu tunavyofahamu, Kamati hii ndio jicho la Baraza katika usimamizi kuhakikisha kwamba utendaji wetu unazingatia kanuni, taratibu, sera, mifumo na miongozo mbalimbali ya kiserikali na ile ambayo inatolewa na Baraza letu la Chuo” amesema Prof. Chibunda

Pia ameelezea dhumuni la mafunzo hayo kuwa ni kuwaongezea uelewa kamati ya ukaguzi na kuwakumbusha majukumu yao na umuhimu wa kamati ya ukaguzi katika kushauri Baraza la Chuo kwenye utekelezaji wa majukumu yao hususani katika usimamizi wa chuo.

Aidha ameongezea kuwa mafunzo hayo yalihusisha pia Menejimenti ya Chuo kutokana na Kamati ya ukaguzi inafanya kazi karibu na Menejimenti hiyo hivyo mafunzo hayo yatawasaidia wote kuelewa pamoja maswala muhimu ya usimamizi wa Rasilimali za Chuo.



Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Prof. Raphael Chibunda akitoa neno la utangulizi wakati wa mafunzo ya kamati ya ukaguzi ndani ya Chuo yalioanza tarehe 28 Octoba 2021

Naye mtoa mada katika mafunzo hayo ambaye ni Muasisi wa  Taasisi ya Ukaguzi wa ndani (TIA) Godfrey Kilenga ameshukuru kwa mualiko alioupata kutoka SUA kutoa mafunzo hayo na kwamba ana Imani yataleta mabadiliko makubwa Chuoni hapa.

Amesema kuwa miongozo mingi ya shughuli za ukaguzi zinatoka serikalini hivyo ni vizuri  wajumbe hao kufanyia kazi yatakayofundishwa ili kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kutimiza malengo waliyojiekea.

Baadhi ya wajumbe na Menejimenti kutoka SUA  waliohudhuria katika mafunzo ya kamati ya ukaguzi.

Story and Photo Credits
Calista Nyimbo - Communication and Marketing 

Share this page