Wanafunzi waonesha ubunifu wa mavazi mbalimbali


Hivi karibuni, wanafunzi wanaosoma shahada ya Sayansi ya mlaji yaani (B.Sc. Family and Consumer Studies) ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) walifanya mazoezi yao kwa vitendo na kuonesha mavazi na  vitu mbalimbali ambavyo ni kazi za mikono yao.

Katika maonesho hayo, wanafunzi wa mwaka wa pili wanaosoma somo la (Cultural Aspects of Clothing) walibuni na kutengeneza mavazi mbalimbali kulingana na makabila na tamaduni za hapa Tanzania. 

Wanafunzi wa mwaka wa tatu kupitia somo la (Costume Design) walitengeneza mavazi mbalimbali yanayovaliwa kwenye matukio na shughuli mbalimbali kwa kutumia vitu vya gharama nafuu vinavyopatikana katika mazingira yetu (Locally available cheap materials).

Tukio hilo lilifanyikia katika ukumbi wa Multipurpose siku ya Ijumaa tarehe 24 Juni 2022 kuanzia saa nne asubuhi na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya chuo.

SUA

Share this page