Tazama Video: Mafanikio Ya Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo (SUA)

 

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kilianzishwa rasmi mnamo tarehe 01 Julai 1984 kwa Sheria ya Bunge Na. 6 ya mwaka 1984. SUA ilipewa Hati Idhini mwaka 2007 chini ya Sheria ya Vyuo Vikuu Na. 7 ya mwaka 2005. Chuo hiki kinatoa wataalamu kuanzia ngazi za Astashahada, Stashahada, Shahada za Kwanza, Shahada za Umahiri na Shahada za Uzamivu.Watalaamu wanaotolewa na SUA hutoa mchango mkubwa katika ujenzi wa Taifa kupitia huduma yao katika sekta mbalimbali serikalini na zile za kibinafsi.

Chuo kimejiwekea malengo ya kimkakati ambayo ni kuongeza udahili wa wanafunzi, miradi ya utafiti na kuboresha huduma za ugani na ushauri wa kitaalamu. Hata hivyo kwa miaka mingi Chuo kilishindwa kufikia malengo hayo kutokana na changamoto mbalimbali zikiwemo uchakavu wa miundombinu na mifumo ya huduma za jamii.

Bofya hapa kusoma kwa undani zaidi mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha mwaka 2015 hadi 2020 (pdf)​​​​​​​

SUA

 

​​​​​​​

Share this page