Tanzia

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Prof. Raphael Chibunda, anasikitika kutangaza kifo cha Mfanyakazi Mwenzetu Prof. Benedicto B. Kazuzuru wa Idara ya Hisabati na Takwimu aliyefariki Dunia tarehe 03.12.2024 katika hospitali ya Mloganzila alikokuwa akipatiwa matibabu.

Mwili wa marehemu utaagwa tarehe 06.12.2024 Dar es salaam na kusafirishwa kuja Morogoro. Msiba upo nyumbani kwake Idiva karibu na shule ya Msingi “Holy Cross”, ambapo mazishi yatafanyika Jumamosi tarehe 07.12.2024 hapa Morogoro katika makaburi ya Kola.


Tuungane kwa pamoja kuifariji familia ya marehemu katika kipindi hiki cha majonzi ya kuondokewa na mpendwa wao.

Bwana ametoa na bwana ametwaa, jina la bwana lihimidiwe, Amina

Tanzia

Share this page