SUA Yasaini Mkataba wa Ushirikiano na Taasisi 7 za Wizara ya Kilimo

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimesaini Mkataba wa Ushirikiano na Taasisi 7 za Wizara ya Kilimo wenye lengo la kukuza uchumi wa Nchi kupitia Sekta ya Kilimo. 

Zoezi hilo limefanyika Februari 9, 2023 katika Kampasi ya Edward Moringe Sokoine mkoani Morogoro ambapo limeongozwa na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu Prof. Maulid Mwatawala kwa niaba ya Makamu Mkuu wa Chuo cha SUA, Prof. Raphael Chibunda.

SUA Yasaini Mkataba wa Ushirikiano na Taasisi 7 za Wizara ya Kilimo

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalam Prof. Maulid Mwatawala akizungumza wakati wa kusaini Mkataba wa Ushirikiano

Prof. Mwatawala amesema wamepata mafanikio makubwa kwa sababu mwanzo SUA ilikuwa na mashirikiano na Taasisi moja ya Wizara ya Kilimo ambayo ni Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) kisha zikaongezeka na kuwa nne(4) ambazo ni TARI, Wakala wa Mbegu Tanzania (ASA)  na Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) na kisha Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC), Mamlaka inayoshughulikia Udhibiti wa Mbolea (TFRA), na Mamlaka ya Afya ya Mimea na Udhibiti wa Viuatilifu) TPHPA.

IMG 1489

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu Prof. Maulid Mwatawala akiweka saini katika Mkataba wa Makubaliano wa SUA na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Kilimo

Amesema kufuatia agizo la Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe wakati wa ziara na Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo chuoni hapo Mkataba huo pia imewajumuisha Vituo vya Mafunzo ya Kilimo (MATI).

Makubaliano yatatuweka karibu ili kutimiza majukumu kwa pamoja lakini pia hayana lengo la kukwamisha jukumu la mtu yeyote tunachosaidiana ni kuisaidia Wizara ya Kilimo katika utekelezaji wa majukumu yakeamesema Prof. Mwatawala.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu TOSCI, Stanford Chijenga Amesema karibu asilimia 90 ya wafanyakazi wao ni wahitimu wa SUA na kila mwaka wanatenga kiasi cha million 70 kwa ajili ya kuwasomesha wanafunzi na zimekuwa zikienda SUA.

Naye Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu Dkt. Sophia Kashenge amesema ushirikiano huu una manufaa makubwa kwao kwa sababu hapo nyuma walikuwa wanafanya kazi kwa pamoja bila makubaliano lakini sasa watafanya kazi na Taasisi hizo kwa umoja na pia wanapokea wanafunzi kutoka SUA jambo ambalo litaongeza wigo mpana wa kufanya kazi.

“Sisi kama wazalishaji wa Mbegu kuna maeneo tulikuwa tunaona tungefanya kazi vizuri tunaamini SUA wana mbegu nyingi ambazo wamezitoa na bado hazijafika kwa wakulima kwa hiyo kwa ushirikiano huu tunaamini tunaweza kuzalisha mbegu kwa pamoja” amesema Dkt. Kashenge

Taasisi ambazo zimeingia makubaliano ni SUA, TARI, ASA, TOSCI, NIRC, TFRA, TPHPA na MATI.

IMG 5008

Baadhi ya viongozi wa Taasisi hizo wakiweka saini katika Mkataba wa Ushirikiano huo

Share this page