Shahada ya Kwanza ya Sayansi ya Misitu, Wanyapori na Utalii SUA washiriki zoezi la usafi chuoni

Katika kuhakikisha mazingira yanakuwa safi na salama kwa viumbe hai pamoja na jamii, wanafunzi wanaosoma Shahada kutoka Ndaki ya Misitu, Wanyamapori na Utalii ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) wameaswa kushiriki katika zoezi la  kufanya usafi kwani jambo hilo ni endelevu na litawasaidia katika masomo yao na hata baada ya kuhitimu.

Shahada ya Kwanza ya Sayansi ya Misitu, Wanyapori na Utalii SUA washiriki zoezi la usafi chuoni

Hayo yamezungumzwa na Mhadhiri Msadizi kutoka Ndaki ya Misitu, Wanyamapori na Utalii Bw. Japhet Mwambusi  ambaye alimwakilisha Kaimu Rasi wa Ndaki hiyo, Dkt. Agnes Sirima katika zoezi la  usafi lilifanyika katika bustani ya mimea yaani  Botanic Gadern katika kampasi ya Edward Moringe iliyopo chuoni hapo .

Amesema wanafunzi wakiwa masomoni washirikiane na jamii pamoja na wadau mbalimbali katika kuhifadhi mazingira  ili  kuzidi kuonesha mchango wao katika shughuli hizo jambo litakalowapatia uzowefu utakao wasaidia mbeleni.

DSC 0280 (2)

Hii inaweza kuwasaidia mara baada ya kuhitimu masomo yao kuweza kuanzisha makampuni yao binafsi  kama vile ya uzalishaji wa miti, uzalishaji wa asali na waweze kuonesha ufaulu mzuri katika masomo yao’’, alisema Bw. Mwambusi

Naye  Mwenyekiti wa Tanzania Forest Students Association (TFSA) Msumi Mkomwa ameeleza kuwa katika zoezi hilo wemeweza kupata elimu juu ya ufugaji wa nyuki na mazo yake uongezaji thamani ya mazao yatokanao na misitu pamoja na  kufanya utalii wa ndege (bird watching).

DSC 0253 (2)

Kwa upande wake mmoja ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza Bw. Asililo Bujimu amewashauri wanafunzi wenzake kutosita kwenda kushiriki katika usafi wa mazingira ili waweze kujifunza vitu mbalimbali ambavyo vitawasaidia katika masomo pamoja na maisha yao mara baaada ya kuhitimu  elimu ya chuo kikuu.

DSC 0370 (2)

 

 

Na Gojo Mohamed - Morogoro

 

Share this page