Rais Samia azindua Jengo Mtambuka la Mafunzo SUA, akimwagia sifa Chuo kwa kufanya vizuri

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amezindua Jengo Mtambuka la Mafunzo lililopo katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) na kukipongeza Chuo hicho kwa kufanya tafiti zenye tija nchini na kutoa majibu kwa mahitaji ya jamii za Tanzania na Afrika.

Rais Samia azindua Jengo Mtambuka la Mafunzo SUA, akimwagia sifa Chuo kwa kufanya vizuri

Akizindua Jengo hilo Agosti 6, 2024 lililojengwa kwa thamani ya Sh. Bilioni 11.7 lenye Maabara 8 na Madarasa 8 yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 3205 kwa wakati mmoja, Rais Samia amekipongeza Chuo Kikuu cha SUA kwa kukamilisha jengo hilo kwa ufanisi mkubwa na kukubali kutoa zaidi ya Sh. Bilioni 2.6 ili kufanikisha ujenzi huo ambapo Serikali imetoa Sh. Bilioni 9 kati ya Sh. Bilioni 11.7 .

pp

“Niseme kwa ukweli nimelemewa na performance ya hapa nilipokuja kuweka jiwe la msingi ilikuwa ni matofali na machuma chuma, pamoja na kwamba nilioneshwa majengo kwenye ramani wakati wananipitisha kunionesha jengo litakuwaje lakini sidhani kama niliamini leo nitakuja kukuta kitu cha aina hii niwapongeze sana sana sana SUA kwa kazi hii nzuri mliyofanya, lakini pia niipongeze Menejimenti ya SUA ama kwa hakika mmefanya kazi nzuri, asanteni sana”, amesema Mhe. Rais Samia.

Rais Samia pia amekipongeza Chuo Kikuu cha SUA kwa kuwa na Maabara hizo mpya zenye ithibati ya kimataifa hali inayopelekea tafiti zinazofanyika kukubalika ulimwenguni kote huku akikipongeza pia kwa kuendelea kufanya tafiti zenye tija, kuzalisha wataalam wanaoendelea kuhudumia jamii pamoja na kufundisha wanafunzi wa kigeni kutoka nchi mbalimbali na kusema kuwa hiyo ni fahari kwa Tanzania .

d

 

“Pia nisema kuwa haya yanayoendelea SUA mnaelekea kwenye kutoa majibu kwa mahitaji ya jamii, mahitaji ya kwanza ajira lakini la pili tafiti mbalimbali zitakazotoa majibu kwa wakulima zinafanyika hapa SUA lakini lingine ni mafunzo kwa vikundi mbalimbali vya nje kuja kujifunza hapa SUA sasa kwa hapa kwa sababu tuna wageni kutoka nchi mbalimbali basi niseme mnatoa majibu pia kwa nchi nyingine ndani ya Afrika , hili nalo nataka niwapongeze sana SUA”, amepongeza Mhe. Samia.

Rais Samia amezindua Jengo hilo ikiwa ni miaka mitano imepita tangu alipoweka jiwe la msingi akiwa ni Makamu wa Rais Agosti 7, 2019.

unnamed (1)

Akizungumza kabla ya kumkaribisha Mhe. Rais Samia, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda amesema Serikali inajivunia sana kazi nzuri za tafiti zinazofanywa na SUA ikiwa ni pamoja na tafiti zilizowezesha kupatikana kwa chanjo ya kuku dhidi ya ugonjwa wa mdondo au kideri na utafiti wa mbegu bora ya maharage inayoitwa Mshindi ambayo inahimili ukame na kustahimili magonjwa .

“Mhe. Rais kuhusu changamoto ya ufadhili ipo, nakumbuka ulitwambia wakati tunapotoa vivutio tuwaangalie na Wahadhiri wa vyuo vikuu ambao wanatumia muda mrefu sana kwa ajili ya kufanya utafiti, tayari tumeanza kutoa tuzo ya Sh, milioni 50 kwa Mtafiti yeyote ambaye utafiti wake utakubalika kimataifa na kigezo cha kimataifa ni kuchapisha majarida ya hali ya juu zaidi duniani, lakini niseme tu ili kuweza kushikilia agenda ya tafiti hatuna budi kutafuta fedha kwa ajili ya kuwawezesha watafiti nchini”, amesema Prof. Mkenda.

2 3 m

 

9 2

 

67

 

unnamed 0

 

o

Na: Farida Mkongwe

Share this page