Wadau wa Bonde la Mto rufiji wametakiwa kuendelea kujizatiti katika kudhibiti shughuli za kibinadamu ambazo zinachangia katika kuharibu mtiririko wa maji ili kuepukana na athari zinazoweza kutokea na kuathiri mahitaji ya maji ya wadau wote wanaotegemea maji hayo.
Wito huo umetolewa na Prof. Japhet Kashaigili ambaye ni Msimamizi na Mratibu wa Mradi wa utafiti wa kutathimini ya mabadiliko ya tabia nchi kwenye bonde la mto Rufiji na kuangalia athari zake katika mtiririko wa maji na utengenezaji wa vielelezo vya kusaidia kupanga mipango ya kimaendeleo katika bonde hilo (UMFULA) wakati wa Mkutano wa kuwasilisha matokeo ya mwisho ya Utafiti huo na kufunga Mradi.